Matokeo ya mechi ya Simba Vs Yanga yapo hapa pamoja na mechi nyingine za Ligi Kuu Sept 26

Jumamosi ya September 26 ni siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania, kwani ndio siku ambayo tumepata nafasi ya kuona mechi ya kihistoria ya watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa uwanja waTaifa Dar Es Salaam.
IMG_1936
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la Amissi Tambwe upande wa mashabiki wa Simba
Kabla ya kuchezwa kwa mechi hiyo ya kihistoria ambapo klabu ya Simba ndio ilikuwa timu mwenyeji wa mchezo huo, Simba na Yanga wamewahi kukutana mara 79, lakini klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kwa mujibu wa rekodi inaonekana kuwa mbabe kwa kuifunga Simba mara 29, huku Simba wakiwa wamewahi kuifunga Yanga mara 23 na kutoka sare mara 27. Hii ndio rekodi ambayo Simba na Yanga ziliingia uwanjani zikiwa zinaijua.
w
Golikipa wa Yanga Ali Mustapha akitoa mpira katika eneo la hatari
Mchezo umemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba, magoli ya Yanga yalifungwa naAmissi Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Malimi Busungu na kuandika goli la kwanza.
434
Mbuyu Twite akitolewa nje na daktari wa Yanga Juma Suphian baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.
Goli la pili lilifungwa na Malimi Busungu kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa SimbaPeter Manyika na kuingia wavuni dakika ya 79. Mechi ilimalizika kwa Mbuyu Twitekupewa kadi nyekundu baada ya kuchelewesha muda ukizingatia alikuwa na kadi ya manjano.
DSC_0087
mashabiki wa Yanga baada ya ushindi wa goli la Busungu
 Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa September 26
  • Coastal Union 0 – 0 Mwadui FC
  • Tanzania Prisons 1 – 0 Mgambo Shooting
  • JKT Ruvu 0 – 1 Stand United
  • Mtibwa Sugar 1 – 0 Maji Maji FC 
  • Kagera Sugar 0 – 0 Toto Africans
Hizi ni pichaz za mechi ya Simba Vs Yanga
DSC_0146
Shabiki wa Simba aliyerusha chupa ya maji uwanjani akiwa kakamatwa na askari polisi
DSC_0105
Hamis Kiiza akimuangalia golikipa wa Yanga aliyechini baada ya kupata maumivu
DSC_0095
Mussa Hassan Mgosi akifanya mipango ya kumpita Mbuyu Twite
DSC_0111
Wachezaji wa Simba na Yanga wakimzonga refa baada ya kufanyiwa faulo mchezaji wa Yanga
DSC_0088
Mashabiki wa Yanga
DSC_0077
Nadir Haroub akimdhibiti Hassan Kessy
DSC_0021
Hamis Kiiza akimkumbatia kocha wake wa zamani Hans van der Pluijm
DSC_0033
Sserunkuma na Jonas Mkude wakiwa benchi

COMMENTS

MICHEZO
Name

BURUDANI ENTERTAINMENT KIMATAIFA KITAIFA MAGAZETI MICHEZO NEWS SPORTS TECHNOLOGY VIDEOS
false
ltr
item
DUNIA KIGANJANI: Matokeo ya mechi ya Simba Vs Yanga yapo hapa pamoja na mechi nyingine za Ligi Kuu Sept 26
Matokeo ya mechi ya Simba Vs Yanga yapo hapa pamoja na mechi nyingine za Ligi Kuu Sept 26
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjyL1WVBQlOyRhJS14C4p9wng793iW51esQCORuKMImnrfiU4aIBMrYCnhIaODumdlMUWt2nxfiTXVeX9spXnUyxj0CFy8mXC6X26mqOzbF_LEVDPfHBd2-VjResVHYQ66Boa_1ZdYLdg/s640/u.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjyL1WVBQlOyRhJS14C4p9wng793iW51esQCORuKMImnrfiU4aIBMrYCnhIaODumdlMUWt2nxfiTXVeX9spXnUyxj0CFy8mXC6X26mqOzbF_LEVDPfHBd2-VjResVHYQ66Boa_1ZdYLdg/s72-c/u.jpg
DUNIA KIGANJANI
https://duniakiganjani.blogspot.com/2015/09/matokeo-ya-mechi-ya-simba-vs-yanga-yapo.html
https://duniakiganjani.blogspot.com/
http://duniakiganjani.blogspot.com/
http://duniakiganjani.blogspot.com/2015/09/matokeo-ya-mechi-ya-simba-vs-yanga-yapo.html
true
8114276925515417542
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy