GEITA Kimenuka Tena..Mtu Mwingine Auwa Kikatili Sababu ya Chuki za Kisiasa...Stori Nzima ipo Hapa


Yadaiwa huenda ni kutokana na chuki za kisiasa zilizosababisha kifo cha kiongozi wa Chadema
Geita. Mtu ambaye hajafahamika jina wala makazi, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Katoro wilayani Geita, baada ya kufikishwa na polisi akiwa hajitambui.
Mtu huyo anasadikika kupigwa na watu wasiojulikana Jumamosi saa mbili usiku, huku tukio hilo likihusishwa na chuki za kisiasa zinazohusiana na vurugu zilizosababisha kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.

Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Daniel Izengo alisema saa 2:30 usiku walimpokea mtu huyo aliyefikishwa na polisi akiwa na majeraha makubwa sehemu za kichwani.
Awali, mganga huyo alisema watu wawili walijeruhiwa katika vurugu zilizosababisha kifo cha Mawazo ambao walifikishwa kwenye kituo hicho wakatibiwa na kuruhusiwa.

Pia alisema watu watatu walifikishwa kituoni hapo juzi akiwamo Mawazo, Elizabeth Paschal (48) na Bahati Michael (38) wote wakiwa wakazi wa Katoro.

Dk Izengo alisema hali ya Mawazo ilibadilika na kumwandikia rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Geita ambako alifariki dunia, huku majeruhi wengine wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa baada ya hali zao kuridhisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Lotson Mponjoli alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea, ikiwamo kuwatafuta watuhumiwa.
Hilo ni tukio la pili ndani ya siku chache, la kwanza likiwa la kifo cha Mawazo.
Chanzo:Gazeti Mwananchi

COMMENTS

MICHEZO
Name

BURUDANI ENTERTAINMENT KIMATAIFA KITAIFA MAGAZETI MICHEZO NEWS SPORTS TECHNOLOGY VIDEOS
false
ltr
item
DUNIA KIGANJANI: GEITA Kimenuka Tena..Mtu Mwingine Auwa Kikatili Sababu ya Chuki za Kisiasa...Stori Nzima ipo Hapa
GEITA Kimenuka Tena..Mtu Mwingine Auwa Kikatili Sababu ya Chuki za Kisiasa...Stori Nzima ipo Hapa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6T4cY-eqbnZZyLu6LvK-Id4yzDsIZybp6fHrXyW-wxl5LEYU1j8-mp-93Dow9GlyoMcYrLOJL9UJ75I6_-kc7ytBxbZovqD_vqauJynJQBTaA19U1wqAS5v3YLo09OlS9IWx8sXxG_xU/s640/1.+achomwa+kisu+na+kufa+mwingine+auawa+na+wananchi+wenye+hasira+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6T4cY-eqbnZZyLu6LvK-Id4yzDsIZybp6fHrXyW-wxl5LEYU1j8-mp-93Dow9GlyoMcYrLOJL9UJ75I6_-kc7ytBxbZovqD_vqauJynJQBTaA19U1wqAS5v3YLo09OlS9IWx8sXxG_xU/s72-c/1.+achomwa+kisu+na+kufa+mwingine+auawa+na+wananchi+wenye+hasira+1.jpg
DUNIA KIGANJANI
https://duniakiganjani.blogspot.com/2015/11/geita-kimenuka-tenamtu-mwingine-auwa.html
https://duniakiganjani.blogspot.com/
http://duniakiganjani.blogspot.com/
http://duniakiganjani.blogspot.com/2015/11/geita-kimenuka-tenamtu-mwingine-auwa.html
true
8114276925515417542
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy