KISIWA PANZA WAMPONGEA SHEIN KUWAPATIA UMEME

WANANCHI wa Kisiwa Panza kiliopo Jimbo la Mkoani, Zanzibar wameanza mikakati ya kujiimarisha kiuchumi baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme kisiwani hapo. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa na ndoto ya kuweka umeme katika kisiwa hicho chenye takribani wakaazi 20,000 mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ili wananchi waweze kufaidi nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa na kukuza uchumi wa pato la mwananchi.
Hata hivyo marais wengi wamepita bila ya wananchi hao kuona mwanga wa umeme hadi mpango huo ulipokamilishwa na Dk Shein. Wakati Dk Shein alipokuwa akiomba ridhaa ya wananchi wamchague ili awe rais wa Zanzibar mwaka 2010 alitembelea kisiwa hicho na kutoa ahadi ya kuwapatia umeme mara atakapoingia madarakani.
“Leo nafurahi kwamba nimetimiza ahadi yangu ya kuleta umeme katika kisiwa Panza.....nilipotoa kauli ya kuleta umeme hapa, wapo baadhi ya watu walinikejeli na kusema huyu Shein anapenda kujipa sifa na mambo makubwa ambayo hawezi kuyatekeleza. …Je, yametimia au bado?”
Shein alihoji na wananchi wakamjibu kuwa yametimia. Dk Shein anasema azma ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ni kuhakikisha kwamba wananchi wazalendo wanaishi katika maisha bora kwa kupata huduma zote muhimu za kijamii.
Anasema kazi hiyo imefanywa kwa kiwango kikubwa ambapo baadhi ya maeneo mengi yamefaidika na huduma hizo ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa za maendeleo zilizoenea sehemu zote Unguja na Pemba hadi vijijini.
Dk Shein amesema amefarijika sana kuona ahadi yake ya kuwapatia wananchi wa Pemba huduma ya nishati ya umeme imetimia hatua ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kubadilisha maisha ya wananchi kuwa bora na kuimarisha uchumi.
“Hiyo ndiyo azma ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kuona wananchi wote wanafaidika na huduma ya nishati ya umeme, maji, shule na huduma za afya kwa jamii yote bila ya ubaguzi,” Shein anaeleza.
Amewataka wananchi wa Kisiwa Panza pamoja na Makoongwe kwa ujumla kuitumia vizuri nishati ya umeme kwa ajili ya maendeleo na kukuza uchumi. Anasema faida za umeme ni nyingi sana ambapo wananchi wanatakiwa kuitumia nishati hiyo kwa ajili ya biashara ikiwemo kuhifadhi samaki kabla ya kupelekwa sokoni.
“Wananchi wa kisiwa Panza na Makoongwe kama mtautumia vizuri sana umeme huu basi unaweza kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo na kiuchumi kwa kuingiza pato binafsi,” anasema Shein. Aidha aliwataka wananchi kutunza miundombinu ya nishati ya umeme ikiwemo nguzo kwa kuacha kuchimba mchanga karibu na maeneo hayo.
Pia aliwataka wananchi kuacha kabisa kujenga nyumba za kuishi au biashara karibu na nguzo kuu zinazopitisha umeme huo kwa sababu ni hatari wa maisha ya binadamu. “Huo ndio ushauri wangu kwenu kuhakikisha kwamba mnalinda mazingira ya miundombinu ya nishati ya umeme ikiwemo kuacha kufanya vitendo vinavyoharibu nishati hiyo,” Shein anasisitiza.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa nishati ya umeme hapo Kisiwa Panza Chokocho Pemba,Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban, anasema usambazaji wa umeme katika visiwa vidogo vidogo vilivyopo Pemba ni miongoni mwa juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuleta maendeleo ya uchumi na kijamii kwa wananchi wake.
Shaaban anasema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kazi hiyo kwa kuleta Pemba umeme wa uhakika kutoka Pangani kwa kuunganishwa na gridi ya Taifa. Anasema baadhi ya visiwa vidogo vidogo kikiwemo Kojani kimefaidika na kupata umeme ambao sasa umewawezesha wavuvi kuhifadhi samaki wao bila ya matatizo wakisubiri kupeleka sokoni.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk Ali Mohamed Shein inachokifanya hapa ni kuendeleza azma ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ya kuwafanya wazalendo wote kufaidi matunda ya Mapinduzi,” anasema Shaaban.
Shaaban anasema kazi ya usambazaji wa umeme vijijini ni mradi endelevu ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha maendeleo yanafikiwa na wananchi kuondokana na umasikini kwa kuitumia nishati hiyo kama mkombozi.
Katika mradi wa usambazaji umeme vijijini tayari Serikali ya Mapinduzi imefanikiwa kufikisha umeme huo katika vijiji Unguja na Pemba. Shaaban anazipongeza nchi washiriki wa maendeleo ikiwemo Norway kwa kushiriki katika miradi ya maendeleo ya Zanzibar Shaaban ambayo ndiyo iliyoanza na mradi wa usambazaji umeme vijijini katika miaka ya 1980.
Anasema Norway imekuwa mstari wa mbele kusaidia maendeleo katika nishati ya umeme ndiyo iliyofanya kazi kubwa ya kukiunganisha kisiwa cha Pemba na gridi ya Taifa kwa kukipatia umeme chini ya bahari kutoka Tanga.
“Tunawapongeza rafiki zetu wa Norway ambao wamefanya kazi kubwa ya kusaidia maendeleo ya nishati ya umeme vijijini Unguja na Pemba na kuleta mabadiliko makubwa,” Shaaban anasema.
Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Mbarouk, anasema Shirika hilo lina mkakati wa kuwapatia wananchi wa Zanzibar umeme wa uhakika ili waweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Anasema kama wananchi wa Kisiwa Panza na Makoongwe watautumia vizuri umeme, unaweza kuleta mabadiliko makubwa ya Mapinduzi ya uchumi na kuongeza pato lao binafsi.
“Wananchi wa visiwa viwili hivi mnaombwa kuitumia nishati ya umeme kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo kwa kuongeza pato la mwananchi,” anasema Mbarouk.
Jumla ya Sh milioni 604,960,764.00 zimetumika katika mradi wa usambazaji wa umeme Kisiwa Panza ambazo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Sh milioni 523,849,410.00 zikitolewa na Shirika la Umeme la Zanzibar.
Jumla ya Sh milioni 363,832,917.00 zimeokolewa na Shirika la Umeme baada ya kazi nyingi zilizostahiki kufanywa na wataalamu wa nje zikifanywa na mafundi wazalendo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa Kisiwa Panza wanasema wamefurahishwa na utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais wa Zanzibar Dk Shein katika kipindi cha kampeni katika mwaka 2010.
“Tunampongeza kwa dhati kabisa Rais Shein kwa utekelezaji wa ahadi zake ambapo lazima tuseme ukweli wengi wetu tuliona kama ni ndoto tu,” alisema Hamadi Juma. Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Sheha ya Kisiwa Panza, Halima Issa mkaazi, anasema uzinduzi wa umeme Kisiwa Panza kwao ni tukio kubwa mbalo hawatolisahau katika maisha yao kwani ni moja ya fursa kubwa ya kupiga hatua ya maendeleo na kupambana na umasikini.
“Tunaipongeza kwa dhati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kutekeleza mradi huu ambao leo hii umeleta faraja kubwa na matarajio yetu kubadilisha maisha yetu na kuwa bora,” anasema Halima.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi na Maji Mustafa Aboud Jumbe anasema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imevuka malengo iliyoweka ya kusambaza na kufikisha nishati ya umeme vijijini Unguja na Pemba ambapo jumla ya vijiji 129 sawa na asilimia 105 ya lengo lililowekwa la vijiji 123 limetekelezwa.
“Shirika la Umeme tumevuka malengo tuliyoweka ya kusambaza nishati ya umeme vijijini Unguja na Pemba kwa mafanikio makubwa huku tofauti ya mjini na vijijini ikiondoka moja kwa moja,” Jumbe anafafanua.
Kuwepo kwa umeme wa uhakika Zanzibar sasa kumeifanya sekta ya utalii kuimarika pamoja na wawekezaji mbalimbali kuonesha nia ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo na uchumi.

COMMENTS

MICHEZO
Name

BURUDANI ENTERTAINMENT KIMATAIFA KITAIFA MAGAZETI MICHEZO NEWS SPORTS TECHNOLOGY VIDEOS
false
ltr
item
DUNIA KIGANJANI: KISIWA PANZA WAMPONGEA SHEIN KUWAPATIA UMEME
KISIWA PANZA WAMPONGEA SHEIN KUWAPATIA UMEME
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgq8wg9p7FjelFsPayAie7XWJpbMxDzLCYP8unw50sLpEOKPR_HOqmrYGreBeDgCZo-CTcuEMh5pupIfJTK4LIPruK6hcoP93g8_6hrt77oz35fT7QttJRRVir4mhCSE2jt-glUgJKqNS8/s640/UME+%25281%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgq8wg9p7FjelFsPayAie7XWJpbMxDzLCYP8unw50sLpEOKPR_HOqmrYGreBeDgCZo-CTcuEMh5pupIfJTK4LIPruK6hcoP93g8_6hrt77oz35fT7QttJRRVir4mhCSE2jt-glUgJKqNS8/s72-c/UME+%25281%2529.jpg
DUNIA KIGANJANI
https://duniakiganjani.blogspot.com/2015/09/kisiwa-panza-wampongea-shein-kuwapatia.html
https://duniakiganjani.blogspot.com/
http://duniakiganjani.blogspot.com/
http://duniakiganjani.blogspot.com/2015/09/kisiwa-panza-wampongea-shein-kuwapatia.html
true
8114276925515417542
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy