Jioni ya October 7 klabu ya Liverpool ya Uingereza ilitangaza rasmi kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha Jurgen Klopp na kujiunga na klabu hiyo, taarifa zilizotoka Ijumaa ya October 8 ni kuwa atatambulishwa mbele ya waandishi wa habari pamoja na kufanya mahojiano na waandishi wa habari.
Jurgen Klopp aliwahi kuwa kocha wa Borussia Dortmund ya Ujerumani kabla ya mwishoni mwa msimu uliyomalizika kuacha kazi na kukaa bila timu kwa kipindi fulani.Jurgen Klopp ametambulishwa Ijumaa ya October 9 hii ikiwa ni siku moja imepita toka asaini mkataba wa miaka 3 wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi, kocha huyo amesaini mkataba wenye thamani ya pound milioni 21.
Jurgen Klopp ambaye alianza kazi ya ukocha katika klabu ya Mainz 05 mwaka 2001 – 2008 ambapo alihamia katika klabu ya Borussia Dortmund. Moja kati ya kauli zinazovutia wengi alizozungumza katika mkutano na waandishi wa habari ni kuwa yeye ni kocha wa kawaida kauli ambayo ilihusishwa kama kijembe kwa Jose Mourinho ambaye anajiita ‘the special one’.
” Ni heshima kubwa kuwa kocha katika moja kati ya klabu kubwa duniani, hii ni fursa kwangu ya kujaribu na kuisaidia klabu, haukuwa muda sahii kwa mimi kujiunga lakini naweza sema ni wakati mzuri kwangu. Sitajiita jina lolote sabau mimi ni mtu wa kawaida na mama yangu anatazama huu mkutano kupitia Tv akiwa nyumbani, ila kama utapenda kuniita jina itakuwa vizuri ukiniita ‘the normal one’ ” >>> Jurgen Klopp