Nahodha wa kikosi cha mpira wa Raga nchini Afrika Kusini Jean de Villiers amestaafu katika raga ya kimataifa baada ya kuambiwa kwamba hatoweza kucheza tena katika mechi za kombe la dunia kutokana na jeraha la taya.
De Villiers anayechezea safu ya kati ya Spring Boks alijeruhiwa katika ushindi wa 46-6 dhidi timu ya Samoa na amelichezea taifa lake mara 109.
Hatua hiyo inamuoroshesha mchezaji huyo wa miaka 34 kama aliyelichezea mara nyingi zaidi taifa lake.
''Raga itadhoofika bila Jean'',alisema mkufunzi wa timu hiyo Heyneke Meyer.''Ni balozi wa kweli wa Afrika Kusini.
De Villiers alisema kuwa alipogundua kwamba anaondoka uwanjani alijua kwamba amecheza mechi yake ya mwisho ya taifa hilo.